Rau Daycare Center

Rau Daycare Center

Rau Daycare Center ni kituo cha kulelea watoto wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) ambacho kipo katika maeneo ya Rau, Moshi. Kituo hiki kilianzishwa na mwanamke wa Kifinilandi. Eneo hili limekumbwa na umaskini pamoja maambukizi makubwa ya virusi vya ukimwi (VVU). Pamoja na kuwa na maambukizi makubwa ya virusi vya ukimwi, watoto wengi wanapata lishe duni. Matibabu kwa wahanga wa VVU mara nyingi hayafanikiwi kama mgonjwa ana hali mbaya kiafya kwa kukosa lishe nzuri.
Kituo hiki cha Rau kilianzishwa kwa misaada kutoka kwa watu binafisi. Matarajio ya kituo yanahafifishwa na ukata wa kifedha. Same Sun NGO inataka kusaidia kituo ikiwa ni pamoja na familia za Rau zinazojitolea

Kituo hiki kinaongozwa na wanawake waishio na virusi vya ukimwi. Upendo Pantaleo anafanya kazi kama mwalimu wa elimu ya awali. Chakula huandaliwa na wapishi wawili, ambao ni Rose Maasimu na Adela Bernad. Binti Juliana mwenye umri wa miaka 16 ambaye naye pia anaishi na virusi vya ukimwi anafanya kazi kama mlezi wa familia. Chakula kinachotolewa katika kituo ni mlo mmoja tu kwa kutwa kwa watoto walio wengi. Kituo kinauwezo wa kuhudumia watoto 30 wenye umri kati ya miaka 3 na 6.

Gharama za kuendesha kituo hiki zinatokana na kufanya malipo kwa viongozi na gharama za chakula. Jengo lenyewe linalotumiwa na kituo limetolewa na taasisi ya Kitanzania inayoitwa TREDO.

Shughuli katika kituo cha Rau huanza saa mbili asubuhi na kumalizika mnamo saa tisa alasiri. Maisha ya kila siku katika kituo cha Rau yanatofautiana sana na vituo vilivyopo Finilandi. Watoto hujifunza kuandika herufi na namba, na hujifunza kiingereza na Kiswahili. Watoto wakubwa huhudhuria katika mafundisho, wakati huo watoto wadogo wakicheza na kuruka katika maboya makubwa. Watoto hupenda musiki, kuimba na kucheza. Mwanasesere hutolewa kama misaada katika kituo na imekuwa maarufu sana.
Licha ya ugonjwa na umaskini, watoto wanafuraha sana. Wageni husalimiwa kwa kukumbatiwa na vicheko vya furaha.

Karibu sana!