Kufadhili Mtoto

Kufadhili Mtoto
Je, ungependa kufadhili mtoto?


Kwa kufadhili mtoto katika kituo cha Rau, utakuwa umesaidia kumpa mtoto mazingira salama na milo miwili kwa siku, pamoja na kuwapa wazazi wao nafasi ya kufanya kazi. Kumfadhili mtoto mmoja hugharimu kiasi cha Tsh 32,000/= kwa mwezi. Kama mfadhili utaweza kuwasiliana na mtoto, na utakuwa ukipokea ujumbe kwa njia ya barua pepe kutoka kwa mtoto unayemfadhili.


Sehemu ya fedha zinazotolewa na mfadhili huelekezwa moja kwa moja katika gharama za uendeshaji wa kituo. Tunafanya hivi, ili watoto wasio na wafadhili wapate nafasi sawa.
Ufadhili wako utaendelea mpaka pale mtoto atakapo anza shule. Kwa wakati huu malipo yako ya kila mwezi yataelekezwa moja kwa moja katika ada ya shule.


Kama unawiwa kufadhili mtoto, tafadhali wasiliana nasi kwa njia ya barua pepe info@samaaurinko.fi.


Asante sana!