Habari

Asanteni kwa mchango kwa miaka iliyopita na Heri ya Mwaka Mpya!
Kampeni zetu za uhamasishaji wa zawadi zilifanikiwa na tuliweza kukusanya zaidi ya Tsh 432,000/= kwa ajili ya watoto. Shukurani zetu za dhati kwa wadau wetu wote!
Asanteni sana.


Mwaka 2012 ulikuwa wa mafanikio sana kwetu. Kiwango cha michango kutoka kwa wanachama kimekua kutoka wanachama 8 hadi 45 wanaolipa. Huu ni mwanzo mzuri kwa mwaka unaokuja!


Uangalizi wa afya za watoto!
Tunatafuta mwangalizi wa afya za watoto kwa kazi za muda katika kituo, ili kukamilisha uangalizi wa afya za watoto wakati wa kazi zao. Kama unawiwa kufanyakazi, tafadhali wasiliana na mwanachama wa bodi kwa taarifa zaidi.