Sama Aurinko kwa Kiswahili

Same Sun ni taasisi isiyo ya kiserikali ambayo ilianzishwa mnamo mwaka 2008 na kikundi cha wanafunzi wa Finilandi pamoja na watu wa Finilandi waishio Tanzania. Taasis hii inakusudia na kulenga kuboresha maisha ya watu wa Tanzania walio katika umaskini uliokithiri kwa kuwajengea uwezo wa kujitegemea kiakili na kimwili.


Kwa sasa Same Sun inafanya kazi na kituo cha kulelea watoto wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) Moshi, nchini Tanzania. Idadi kubwa zaidi ya mama wa watoto hawa nao wameathirika pia na virusi vya ukimwi, na taasisi hii huwasaidia kugharimia elimu yao na mafunzo ya kiingereza.


Mwakilishi wetu nchini Tanzania ni ndugu Hanna Metson. Yeye hufanya kazi na kampuni iitwayo Tanzania Volunteers, kwa kuratibu mafunzo kazini kwa wahitimu wa chuo na kazi za kujitolea katika kituo cha kulelea watoto.


Unaweza kupata taarifa na habari zinazojili za Same Sun katika ukurasa wetu wa Facebook, ukurasa wetu wa Facebook utaupata kwa jina la Sama Aurinko ry / Same Sun NGO